Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Cheed na Killy waibukia Konde GangCheed na Killy waliozua gumzo mitandaoni  siku za nyuma  mara baada ya kutoka Kings music kwa kuandika ujumbe unaofanana katika kurasa zao za instagram kwa kudai kuwa wametoka kings music kwa sababu za kifamilia.


Hatimae hatima yao imejulikana  hapo jana mara baada ya kujiunga na Konde Gang iliyoko chini ya Konde Boy Harmonize,mpaka sasa konde Gang imefikisha idadi ya wasanii wa nne  waliopo chini ya lebo hiyo ambao ni Ibrah, Skales, Killy  na Cheed.


Kama kawaida yao Cheed na Killy wameandika ujumbe mrefuu  unaofanana katika kurasa zao za instagram kuwataarifu watanzania na mashabiki zao kuwa sasa ni wasanii wa Konde Gang iliyoko chini ya Harmonize.


Kupitia ukurasa wake wa instagram meneja wa Harmonize Mjerumani amewakaribisha kwa kuandika ujumbe ambao ulikuwa unasomeka hivi.


 "lengo letu ni kuwapa fursa vijana wenzetu wa kitanzania wenye vipaji ili kwa pamoja kuutangaza mziki wa Tanzania,Afrika na duniani na kumaliza kwa kusema karibuni cheed na killy kwenye familia ya Konde Music World ward".

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments