9/22/2020

Country Boy Atoboa Siri ya Kusota Konde Gang "Nipo Konde Gang tangu miezi 11 iliyopita"

 


Baada ya kupewa gari kutoka katika lebo ya Konde Gang msanii Country Boy amefunguka kuwa alikuwepo kwenye lebo hiyo tangu miezi 11 nyuma kabla ya kutambulishwa kwake siku kadhaa zilizopita.

 


Akifunguka suala hilo  kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio inayorushwa kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa 7:00 mchana hadi 10:00 jioni Country Boy ameeleza kuwa 


‘‘Mara ya mwisho kuachia kazi yangu ilikuwa ni Album ya Yule boy, baada ya kuachia hiyo nilikuwa nimejipanga kwa ajili ya hii EP yangu halafu ujue mimi nilikuwepo pale Konde Gang kama miezi 11 iliyopita kabla ya kutambulishwa ’’


Pia Country Boy amewapa sifa kundi la OMG kwa kusema huu ndiyo wakati wao wakutamba kwani HipHop ya Tanzania inatakiwa kufika hadi nchi za nje, ‘‘Hasira ambayo wanayo OMG ni kubwa sana kwenye huu muziki na HipHop ya Tanzania inatakiwa itoke nje kwa hiyo huu ndiyo muda wao, mfano kama Young Lunya alipata ushawishi kutoka kwa Chidi Benz"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger