Dada wa Shilole Alivyoteseka Kuolewa na HarmorapaDada wa msanii Shilole ambaye amejitambulisha kwa jina la Khadija Ziota ameeleza kuwa amepitia wakati mgumu na kuteseka wakati anataka kuolewa na msanii Harmorapa kwani mwanzo alikuwa anamkataa.

Khadija Ziota amesema Harmorapa alikuwa ni mtu wa kumkimbiakimbia mpaka alipojaribu ku-force na kumuhangaikia hadi imewezekana wao kuoana.

"Harmorapa alikuwa mtu wa kunikimbiakimbia siku zote mpaka nilipojaribu ku-force na kumuhangaikia hatimaye imekuwa hivyo, alikuwa ananikataa kwa muda mrefu halafu haeleweki mara kugeugeua ila nimetumia nguvu nyingi sana na kupambana ili kumpata ikiwemo pesa"

Kwa upande wa Harmonize amesema sababu ya kumkataa mwanzoni mwanamke huyo ni kutokana na uzuri wa rangi yake na alikuwa haamini kama atakuwa peke yake.

Wanandoa hao wapya mjini wamesema wamemaliza fungate yao "honeymoon" na wapo tayari kujibu maswali ya watu ambao wanawauliza ikiwemo kufunga ndoa ya siri

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments