9/28/2020

Dada wa Usafi Anaswa na Dawa za KulevyaMAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imemkamata Maria Edson Mtambo (25) Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 448.12 kuelekea nchini India.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema, kuwa binti huyo ni mfanya usafi huko Tegeta, na aliyekuwa anamtumia dawa hizo ni mpenzi wake raia wa nje.

Kamishna Kaji amesema kuwa dawa hizo alizihifadhi katika kifurushi cha vitabu viwili ambavyo ndani yake kuliwekwa unga wa dawa hizo.

Aidha, Kaji amewataka vijana kuwa makini na raia wa nchi za Magharibi kwa usalama zaidi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger