'Dawa za Kuongeza ‘Hips’ Zilivyotibuka na Kuniharibia Figa Yangu' Mwanamke ajutia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Shinikizo za kutaka kuwavutia wanaume zimewafanya wanawake kujipata wakifanya vitu hatari katika miili yao. Kuanzia kuchubua ngozi zao ili kuonekana kama wazungu hadi kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha muonekanao wa viungo vyao mbalimbali .

 Dora Kemunto ni miongoni mwa waliojibadilisha  kutumia dawa nyingi zinazouzwa  ili kuongeza sehemu mbalimbali katika miili ya wanawake ili kuwavutia wanaume. Baada ya kuarifiwa na rafiki yake kuhusu dawa ya kuzidisha  ukubwa wa makalio yake na  kiuno. Alipewa mseto wa tembe na kemikali  ambazo alitakiwa kupaka katika sehemu ya kiuno ili kuipanua sehemu hiyo. Baada ya miezi miwili alifaa kuona mabadiliko lakini kilichotokea kilimshangaza na kumpa hofu. Sehemu yake moja ya kiungo ilianza kuwa kubwa kuliko ya pili na umbo lake likajipinda akawa kama mlemavu.

 Pia sehemu yake moja  ya makalio ilikuwa kubwa kuliko nyingine. Hatua hiyo ilimfanya kwenda hospitalini lakini madaktari wakasema  dawa alizopewa zilikuwa  na kekimali mbaya ambazo  zilichoma sehemu ya mafuta na nyama za mwili wake na hivyo basi kumpa ulemavu. Alitakiwa kufanyiwa upasuaji ambao hauwezi kutekelezwa humu nchini na anahitaji shilingi milioni nne kwenda Brazil ambako wana uwezo wa kumfanyia upasuaji wa kulirekebisha umbo lake.

 Dora anashangaa mbona dawa hizo zilimharibikia ilhali aliyempa amezitumia kwa muda mrefu na  hajawahi kuharibikiwa au kulalamika. Madaktari wamemwambia kwamba kuna hatari nyingine za kiafya ambazo huenda atazipata siku zijazo  kwa sababu dawa hizo zina kemikali zinazopenyeza hadi katika sehemu nyingine muhimu za mwili kama vile moyo na mishipa. Dora amejaribu kupata  usaidizi kutoka kwa waliomuuzia dawa hiyo lakini wamemkwepa huku  mmiliki wa duka alikonunua mchanganyiko huo akidai kwamba Dora anafaa kujilaumu kwa sababu hakufuata maagizo ifaavyo wakati akizitumia dawa hizo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad