9/17/2020

Diamond Platnumz kawapeleka wafanyakazi wake Wasafi Village baada ya kufungiwa kwa siku 7

 
Hiv karibuni wasafi FM ilifungiwa kutokana na kosa la Baba levo kuongea lugha fulani ambayo sio nzuri kwenye kipindi. Baada ya media kufungiwa boss wao Diamond Platnumz ndo kwanza akawapeleka Wafanyakazi wake wote wa media sehemu ya kula bata na kurelax hiyo sehemu wakaiita "Wasafi village" na ilitegemewa labda akasirike au ampanish Baba Levo lakini ikawa tofauti.


Baada ya kufika hilo eneo Diamond akatoa speech kwa wafanyakazi wake kwanini amewaleta hapo namnukuu " baada ya sisi kufungiwa najua itakuwa imewaudhi kikubwa lakini nimewaleta hapa Ili mtulize akili zenu lakini nitawaleta maofisa wa TCRA kutoa elimu kwenu na taratibu za kanuni za media ili next time lisijirudia Tena".


Baada ya hapo akamwita Baba Levo aombe msamaha kwa watanzania na kwa wafanyakazi wake ili kuweka mambo sawa.


Maisha ya wafanyakazi wa Wasafi kwenye Wasafi Village wamekuwa wakirusha live kupitia YouTube pamoja na Wasafi Tv ambako hapajafungiwa. Nimependa sana hii idea inatufanya tujue tabia za wakina George Ambangile nje ya kuchambua mpira anakuaje? Binti Suleiman Yuko VIP n.k


Binafsi nimependa vimbwanga vya mzee Mbwela huyu mzee ana vituko Sana pamoja na Baba Levo.


N.B Namna alivyofanya Diamond inasaidia Sana wafanyakazi kutengeneza bond lakini pia kujuana zaidi ndio namna ambavyo boss uwe hivyo. Hii pia inasaidia mfanyakazi kujisikia anajariwa.


Big up kwa hii kitu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger