9/10/2020

Diana Rigg wa 'Game of Thrones' afariki duniaMsanii maarufu wa filamu nchini Uingereza, ikiwemo series ya "Game of Thrones" Diana Rigg amefariki dunia siku ya leo akiwa na umri wa miaka 82 kwa ugonjwa wa Saratani. 


Diana Dame Rigg 82 alipata umaarufu kupitia filamu zake Bond girl, On her Majesty, Secret na katika series ya Game of Thrones ambapo aliigiza kama Olenna Tyrell. 


Kwa mujibu wa msemaji wake amesema kifo chake kimemkuta nyumbani na familia yake asubuhi ya leo,  ambapo hakuamka mpaka walipofikia hatua ya kumuamsha na kugundua kwamba amefariki. 


Aidha Msemaji huyo ameviomba vyombo vya habari kumpatia nafasi ya kutozungumza chochote muda huu kutokana na mambo ya kifamilia hasa katika kipindi hiki kigumu. 


Diana Rigg alizaliwa Julai 20, 1938 katika Mji wa Doncaster, Kusini mwa Yorkshire nchini Uingereza.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger