9/13/2020

Dr Bashiru Awashangaa Wapinzani, Atoa Maagizo Kwa Wasanii Nchini...


NUKUU ZA KATIBU MKUU KWENYE MKUTANO WA KAMPENI MVUMI. 

"...Ukitoka Bukoba na MV Viktoria ukapanda Mwanza SGR unalala Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Baada ya SGR kukamilika, watu watatoka Dodoma, wanakwenda kufanya shughuli zao Dar es salaam na kurudi kulala hapa Mvumi." Dkt. Bashiru


 "Sasa wao wanasema eti SGR haina uhusiano na maisha ya watu, nadhani hao watu wanaowasema ni wa sayari nyingine ambayo hatujaijua na hao ni wagunduzi wakubwa nadhani wamegundua sayari  ya watu wapya." 


"Sayari imegunduliwa na vyama vyama upinzani ambapo wanaishi watu wasiohitaji simu, wasiohitaji ndege, wasiohitaji umeme, wasiohitaji barabara za lami na watu wa aina hiyo watakuwa ni watu wanaoishi Kijima." Dkt. Bashiru

"Tunawataka wasanii wote waliotuunga mkono, wiki moja kabla ya tarehe 28 Oktoba, 2020, waanze kutunga nyimbo za kushangilia ushindi wa kishindo, hizi nyimbo za kuelimisha ziendelee, kuanzia tarehe 20 Oktoba, 2020 tungeni nyimbo za upendo, amani, furaha, nyimbo za pongezi kwa Dkt. John Pombe Maguguli."
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger