Fatma Karume Afukuzwa Kazi...Kisa Hichi Hapa

advertise hereMWANASHERIA na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini, Fatma Karume, amefukuzwa katika Kampuni ya Uanasheria ya IMMMA Advocates aliyoshiriki kuianzisha

Akieleza kufukuzwa kwake, Fatma ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya sasa, anahusisha tukio hilo na kile alichokiita ‘uovu’ unaotokana na harakati zake.

“Hii ni kuwajulisha nyote kwamba, nimefukuzwa kwenye ofisi niliyoijenga. Uovu wangu, uanaharakati,” ameandika Fatma kwe nye ukurasa wake wa twitter leo tarehe 21 Septemba 2020.

Mwanaharakati huyo ameuambia mtandao huu, kwamba kabla ya kampuni hiyo kumchukuliwa, ilimuandikia ya barua ya onyo ikimtaka kuacha mara moja shughuli za uanaharakati, na kwamba asipofanya hivyo, angefukuzwa.


“Nafikiri kwa kuniondoa mie watapata kazi zaidi, kwa hiyo suala ni kwamba ni kunifukuza mimi ili wapate kazi nyingi,” amesema Fatma na kuongeza:


“Sababu kuu ya kunifukuza ni uanaharakati wangu, na waliniandikia kabisa kwenye barua kabla ya hatua hii, kwamba niache harakati zangu la sivyo watanifukuza.”


Kwa mujibu wa barua iliyotolewa tarehe 16 Septemba 2020 na Sadock Magai, Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo, Fatma ameondolewa katika sehemu ya umiliki wa kampuni hiyo baada ya mkataba wake alioingia tarehe 26 Machi 2007 kuvunjwa.


Barua hiyo inaeleza kuwa, mkataba wa Fatma kuwa sehemu ya mmiliki katika kampuni ya IMMMA Advocate, umevunjwa tarehe 16 Septemba 2020, baada ya washirika wenzake kufika makubaliano ya kuvunja ushirikiano naye.

“Washirika wenzio walikutana tarehe 16 Septemba 2020, kujadili na kuamua kwamba hawataki tena kufanya biashara na wewe. Washirika wenzio wameamua kukuondoa kama sehemu ya mmiliki na kuvunja mkataba wako kuhusu maslahi yako yote katika kampuni,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Aidha, barua hiyo imemtaka Fatma kukabidhi ofisi ndani ya siku 30, tangu siku ya uamuzi huo kutolewa. “Ndani ya siku 30 tangu kutolewa kwa maamuzi haya, tunakuomba ukabidhi kila kitu ambacho kiko mikononi mwako,” inaeleza barua hiyo.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE