google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Grealish aongeza mkataba Aston Villa, je ni pigo kwa Man United ? | UDAKU SPECIAL

Grealish aongeza mkataba Aston Villa, je ni pigo kwa Man United ?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Kiungo huyo raia wa England mwenye umri wa miaka 25 ambaye alijiunga na Aston Villa akiwa na umri wa miaka nane pekee amesaini mkataba huo hii leo ambao utamfanya aendele kusalia Villa kwa miaka mitano zaidi. Na hivyo utamfanya kulipwa mshahara wa paundi 140000 kwa wiki kutoka paundi  70000 alizokuwa akizipata hapo awali.


“Ni klabu yangu, hapa ni nyumbani na najisikia furaha hapa.” amesema Grealish


Grealish amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Manchester United katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi ambalo lipo wazi mpaka Oktober 05, lakini klabu ya Aston Villa imempa thamani ya fedha za Uingereza pauni milion 80 kama ada ya uhamisho kiasi ambacho Manchester United hawapo tayari kulipa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad