9/21/2020

Harmonize Anawasha Moto Mpaka Zimbabwe – King 98MSANII kutoka nchini Zimbabwe, King 98, amefunguka kuhusu kufanya kolabo na msanii na Boss wa Konde Gang, mtu mzima Harmonize, pia ametaja watu anaowapa nafasi kwenye maisha yake.

King 98 amesema anataka kufanya kazi na Harmonize kwa sababu hata nchini kwao Zimbabwe wapenzi wa muziki wanamkubali sana.


“Kufanya kolabo na Harmonize sio kitu kibaya, na kizuri zaidi ni msanii mkubwa ambaye hata nchini kwetu watu wanamkubali hivyo ningependa nifanye naye kazi,” amesema King 98.

Aidha akizungumzia kuhusu maisha yake binafsi nje ya muziki, King 98 ameeleza kuwa; “Vitu ninavyopata maishani mwangu ni baraka, siwezi kuwapa watu nafasi kwa ajili ya vitu vingine, nafanya kazi ili watu waone, muda wangu mwingi natumia kwa ajili ya mama yangu, na mpenzi wangu na mtu ambaye ananishawishi ni baba yangu.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger