9/16/2020

Wafahamu wasanii 5 waliozawadiwa kofia na Rais Magufuli kwenye kampeni, wakiwemo Alikiba, Diamond na HarmonizeHawa ndio wasanii watano walibahatika kuzawadiwa kofia na Mh. Rais Magufuli wakati wa kampeni zake zinazoendelea mikoani. Tukio la msanii Alikiba la kupewa kofia leo limefanya idadi ya wasanii waliopewa kofia na Rais Magufuli kufika watano na kadri siku zinavyoenda huenda tukaona wasanii wengine wakapewa kofia na Rais kwani kampeni bado zinaendelea.Msanii wa kwanza kabisa ni Mrisho Mpoto na wapi ni Bnana Zoro, wasanii hawa wote wawili walipewa kofia na Rais Magufuli katika kampeni zake zilizofanyika mkoani Singida ambapo wote wawili walipewa kofia kwa wakati mmoja.


Tukio la pili la msanii kupewa kofia ni Diamond Platnumz katika kampeni zilizofanyika mkoani Mwanza ambapo ndio tukio lilovuta hisia za watu wengi kutokana na Diamond alivyotoa shukrani kwa Rais hadi kupelekea kwenda kuihifadhi kofia hiyo kabatini.


Tukio la tatu ni msanii Harmonize ambalo lilifanyika katika kampeni za mkoani Geita katika wilaya ya Chato ambali lilifanyika wiki hii siku ya jumatatu.


Na tukio la nne ni la msanii Alikiba ambaye amepewa kofia yake mkoani Kagera wakati Mh. Rais anafanya kampeni za kuomba kura, kwahiyo Alikiba, Diamond Platnumz, Harmonize, Mrisho Mpoto na Banana Zoro ndio wasanii waliobahatika kupewa kofia na Rais Magufuli.


Unahisi ni kwanini wasanii Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize matukio yao yamevuta hisia za watu wengi kuliko tukio la mjomba Mrisho Mpoto na mkongwe Banana Zoro -?

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger