9/16/2020

"Inaniuma Kuitwa Mbeba Pochi wa Wema Sepetu" - Petitman Afunguka

 
Meneja na mjasiriamali Petitman Wakuache amefunguka kuwa alikuwa anaumizwa na maneno ya watu mitandaoni kiasi kwamba kufikia hatua ya kuchanganyikwa kwa watu kumuita mbeba pochi wa Madam Wema Sepetu.


Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Petitman Wakuache amesema urafiki wake na Wema Sepetu umedumu kwa miaka 15, hivyo kwa sasa hata watu wakimtukana watakuwa wanajisumbua bure kwani hakuna tusi jipya.

"Zamani nikitukanwa mitandaoni ilikuwa inaniuma sana hadi nachanganyikiwa siku nzima kuanzia kuitwa mbeba pochi wa Madam Wema Sepetu lakini sasa hivi hata siumii kwa sababu hakuna tusi jipya" amesema Petitman Wakuache

Aidha ameongeza kusema "Madam Wema Sepetu anapambana sana, inaweza kupita hata wiki 2 bila ya kuonana kwa sababu anarekodi filamu yake, urafiki wetu unaenda mwaka wa 15 sasa, upande wa mwili wake sioni kama ni tatizo ikiwa yeye mwenyewe anaufurahia na kuupenda"
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger