9/24/2020

Je Ufalme wa Messi, Ronaldo umefikia mwisho ?, wakosekana hadi 3 bora tuzo za UEFA

 

 


Katika hali isiyo ya kawaidi huwezi kutarajia kuwa msimu wa mwaka 2019/20 wachezaji ghali, bora kabisa duniani na wenye mafanikio makubwa kunako soka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wasingeliweza kukosekana hata tatu bora katika tuzo za mchezaji bora wa mwaka zinazotolewa na UEFA (UEFA Player of the Year Awards).

 

Lakini hilo limewezekana, mapema hii leo siku ya Jumatano UEFA imetoa orodha ya majina matatu ya wachezaji ambayo ndiyo yameingia kwenye tatu bora kuwania tuzo hiyo na kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya Mwongo mmoja kupita majina maarufu na yaliyozoeleka katika kuzichukua tuzo hizi, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekosekana.

 

Majina ya wachezaji Robert Lewandowski na Manuel Neuer kutokea Bayern Munich, na latatu likiwa ni la kijana wa Manchester City, Kevin De Bruyne ndiyo yaliobahatika kuingia tatu bora na hatmaye kupatikana mchezaji bora wa mwaka kwenye tuzo zitakazotolewa siku ya Alhamisi ya tarehe 1 Oktoba.


Nyota huyo wa Barcelona, Messi ametwaa tuzo hizo katika mwaka 2010-11 na 2014-15 na jina lake limeingia kwenye kinyang’anyiro hicho zaidi ya mara sita ndani ya misimu 10.


 

Wakati kwa upande wa Ronaldo amejibebea tuzo hiyo zaidi ya mara tatu 2013-14, 2015-16 na 2016-17 na kipindi chote hiko alikuwa akikitumikia kikosi cha Real Madrid. Na ameingia kwenye kinyang’anyiro hicho zaidi ya mara tisa, na kunako msimu wa aliingia hadi kwenye nafasi ya pili 2017-18 na mara tano akishika nafasi ya tatu.

 

Katika tuzo hizi Orodha ya wachezaji watatu ambao wanawania mchezaji bora wa mwaka wa UEFA huwa wanachaguliwa na Makocha 80 wa vilabu vilivyoshiriki hatua ya makundi ya UEFA Champions League na UEFA Europa League msimu wa 2019/20, Waandishi wa habari 55 kutoka katika kila vyama ambavyo ni mwanachama wa UEFA wakichaguliwa na na kikundi cha Vyombo vya Habari vya Michezo vya barani Ulaya (ESM).


Imeandikwa na Hamza Fumo, Instagram @fumo255

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger