google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lamshikilia kijana wa miaka 32 kwa tuhuma za mauaji | UDAKU SPECIAL

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lamshikilia kijana wa miaka 32 kwa tuhuma za mauaji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Bariki Kajuni mwenye miaka 32 ambaye ni mkazi wa  Makambako, Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za kosa la mauaji ya Ansalemo Stawi Kisheria .
Ansalemo Stawi Kisheria alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Zahanati ya Isangawana kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtuhumiwa.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendelea na msako na mnamo tarehe 10.09.2020 majira ya saa 17:30 jioni huko Kitongoji na Kijiji cha Mgololo Mufindi, Wilaya ya Mafinga, Mkoa wa Iringa askari Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na askari wa Mafinga walimkamata mtuhumiwa".

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad