9/21/2020

Jokate Aagiza Uchunguzi Ukamilike Upesi Kuhusu Tuhuma za Wachina
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo Jokate Mwegelo ameagiza kukamilika haraka kwa uchunguzi dhidi ya Wachina watatu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kukwepa kodi ya Tsh.Bilioni 2.5 >> “wamekwepa kodi Vingunguti na Mwenge, wakaja kujificha Kisarawe, tumewanasa”

Tayari Polisi Wilayani Kisarawe wanawashikilia Wachina hao waatatu ambao wanadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa kipindi cha kuanzia Januari 2018 hadi August 2020 kupitia Kampuni zao ambazo ni Tongda Venture LTD na Onething Limited zinazojishughuliaha na uchimbaji na usafirishaji wa Madini aina ya Kaolin.

“Bil 2.5 ni parefu sana, hapa Kisarawe tungepata Hospitali nyingine moja ya Wilaya na vyumba vipya vya Madarasa zaidi ya 50, haiwezekani Rais Magufuli anahangaika kusogeza huduma kwa Wananchi, halafu Watu wanakwepa kodi na wapo ndani ya Kisarawe, naelekeza vyombo vyote husika kuanzia TRA, Jeshi la Polisi, Uhamiaji Kisarawe, wahakikishe uchunguzi unakamalika mara moja na pesa zitolewe zote, hizi pesa ni za Watanzania” – Jokate

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger