9/14/2020

Jose Mourinho, Klopp Waungana


BOSI wa Tottenham, Jose Mourinho amemuunga mkono kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kwa kuzishangaa timu ambazo zinatumia kiasi kikubwa cha fedha katika usajili huu badala ya kujenga timu.Klopp hivi karibuni alisema kuwa hawezi kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye usajili kama ilivyo kwa timu za Chelsea na Manchester City zaidi yeye anaboresha kikosi chake kuwa cha ushindani.Msimu huu klabu nyingi za Ulaya pamoja na kote duniani zimeyumba kiuchumi hasa kutokana na janga la virusi vya corona ambalo limesababisha uchumi kushuka. Mpaka sasa Klabu ya Chelsea imetumia kiasi cha pauni 250m katika usajili wake kwa kuwasajili Hakim Zieych, Ben Chilwell, Kai Havertz, Timo Werne, Thiago Silva na Malang Sarr.Mourihno alisema:“Nakumbuka Jurgen alisema kuwa Liverpool siyo timu ya mtu bali ni ya watu wote, hivyo haina tofauti na Spurs kwa hiyo hatuwezi kuingia soka tu na kumwaga fedha kwa ajili ya kusajili lazima tuwe na mipango.“Ndiyo tumeweka bidii ya kujijenga upya na nataka watu wanielewe vizuri ndani ya kikosi changu kwa sasa nahitaji straika mmoja tu kuongeza nguvu,” Liverpool kwa msimu huu mpaka sasa wamesajili mchezaji mmoja ambaye ni Kostas Tsimikas, huku Spurs ikitumia pauni 30m kuwasajili Pierre-Emile Hojbjerg, Matt Doherty na Joe Hart.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger