JPM Aanika Siri ya Chenge, Amwambia Kazi Zipo Nyingi TuMGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Magufuli amemweleza aliyekuwa mbunge wa Bariadi Mkoa wa Simiyu, Andrew Chenge,  kuwa asiwe na wasiwasi kwa kukosa ubunge kwani bado kuna vyeo vingi serikalini.

Amesema hayo leo, Agosti 4, 2020, wakati akiendelea na kampeni za kuwania nafasi hiyo na kuwatambulisha madiwani na wabunge wa chama hicho katika mji wa Bariadi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika Oktoba 28, mwaka huu.

“Nimezungumza Shinyanga na maeneo mengine, kazi zipo nyingi, Mzee Chenge ‘Mtemi’ ni kaka yangu kwelikweli, nilipoingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1995 mke wangu alikuwa na mimba, aliyenisaidia pesa za kwenda hospitali ni Chenge.  Huu ndiyo ukweli,” alisema  na kuongeza:

“Mheshimiwa Chenge kazi zipo nyingi mno hata utemi nao ni kazi kubwa tu.  Bariadi achaneni na maneo ya upinzani, leo nataka niwaite wote watatu; Andrew Chenge (Bariadi), Dkt. Chegeni (Busega) na Salum Mbuzi (Meatu) waniombee kura hapa. Njooni hapa wote.


Naye Chenge, akizungumza baada ya kuitwa na Magufuli, alisema, “Mheshimiwa Rais nakushukuru sana, sikutegemea kama histioria hiyo ya mwaka 1995 ungeisema mbele ya wananchi hawa, nakushukuru sana na ninamshukuru Mama Janeth kwa moyo wake wa upendo.

“Tutahakikisha tunapata ushindi mkubwa wa kura zako.  Namhakikishia kijana wetu Engineer Kundo, mimi na Komando Suzy tutafanya kazi ya uhakika kuhakikisha kura za mbunge zinatosha, za madiwani 31 zinatosha, japo tayari madiwani wamepita bila kupingwa lakini hatubweteki.

“Mheshimiwa rais wewe ni mtemi wa Tanzania, tunatekeleza tu matakwa ya katiba, isingekuwa hivyo basi tayari wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Umeitendea haki Simiyu na Tanzania.”

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments