9/23/2020

Kambi ya West ham United yakumbwa na CoronaTaarifa za ndani za klabu ya West Ham United maarufu wagonga nyundo wa London zinaeleza kuwa Meneja wa timu hiyo David Moyes sambamba na wachezaji wawili wameambukizwa virusi vya Ugonjwa wa Corona COVID-19.


Mapema asubuhi ya leo West Ham wameutaarifu umma kuwa mchezaji Issa Diop sambamba na Josh Cullen pamoja na Meneja Moyes walibainika kuambukizwa COVID-19 baada ya vipimo kufanyika katika kujiandaa na mzunguko wa tatu wa kombe la Carabao dhidi ya Hull City hapo jana


"Timu ya madaktari walitaarifa kuhusu matokeo ya vipimo wakati timu hiyo ilipokuwa katika uwanja wa mazoezi wa London kujiandaa na mchezo wa Jumanne jioni katika mzunguko wa tatu wa Michuano ya Carabao dhidi ya Hull City. Meneja sambamba na wachezaji hao tayari wameshaachana na kambi na kurejea nyumbani."


Mwisho timu hiyo imewatakia kupona haraka, hata hivyo Meneje msaidizi Alan Irvin alikaimu majukumu ya timu hiyo na matokeo ya mchezo wa jana usiku West Ham waliibuka na ushindi wa 5-1, Sebastien Haller na Andriy Yarmolenko wamefunga mabao mawili kila mmoja wakati Robert Snodgrass akitamatisha kalamu hiyo ya magoli


Irvin amenukuliwa akisema "Majira ya saa 12:20 jioni punde tulipokea taarifa kutoka kwa daktari wetu na kutueleza kuwa watu wetu watatu muhimu katika timu wameambukizwa COVID-19 Meneja na wachezaji wawili."


 


TOP STORIES


CURRENT AFFAIRS

Nkurunziza afariki dunia, chanzo chatajwa


CURRENT AFFAIRS

RC Mbeya awatimua Kidato cha 5 na 6 awataka kurudi


ENTERTAINMENT

Seyi Shay ataja orodha ya wanaume alio-date nao


CURRENT AFFAIRS

Kama alivyosema Makonda ''Wameoga'' - KamwelweMOST POPULAR


CURRENT AFFAIRS

Fahamu jinsi Mtwara ilivyompa Zitto uchungu


CURRENT AFFAIRS

Maalim Seif amuunga mkono Tundu Lissu


CURRENT AFFAIRS

Ndugai kutoa 'bonus' endapo Magufuli atachaguliwa


LIFE & STYLE

Wakazi wa Vijibweni, Dar wahofia Mamba baharini


CURRENT AFFAIRS

Magufuli ataja kilichowaponza Kaliua


 

ABOUT US

ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS

NETWORK

IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO

© 2020 East Africa Television Limited. All Rights Reserved


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger