9/03/2020

Kauli ya Gareth Bale Kuhusu Kurejea EPLWinga wa Kimataifa wa Wales,Gareth Bale amesema atafikiria kurejea katika Ligi kuu ya England iwapo Klabu yake ya Real Madrid itamruhusu kuondoka katika viunga vya Santiago Bernabeu.

Bale ameulaumu uongozi wa Real Madrid kwa kutomruhusu kuondoka mapema iwezekanavyo huku akionyesha furaha kwa kupewa thamani na Timu yake ya Taifa ya Wales.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 alikaribia kutua katika moja ya Klabu ya nchini China lakini mpango huo ulizuiliwa katika dakika za mwisho katika usajili wa miaka ya hivi karibuni iliyopita.

Bale alicheza michezo ishirini pekee katika mashindano yote na alishiriki katika mechi mbili tu tangu kurejea kwa ligi baada ya likizo ya dharula iliyosababishwa na janga la Corona.

Akizungumza akiwa katika maandalizi ya Timu yake ya Taifa ya Wales inayokabiliana na Finland mwenye michuano ya UEFA National League, Bale amesema''Kila mmoja anajua namna ambavyo nafurahia kuja kuichezea Wales ,sehemu ambayo mashabiki wako wanakupa thamani yako pasipo kujalisha upo katika hali gani kiuchezaji''

''Nilijaribu kila kitu ili niondoke kwa kuwa bado ninahitaji kucheza,lakini kila kitu kilizuiliwa,na kila kitu kipo chini yao na ndio wanaonimiliki na bado nina mkataba na Real Madrid hivyio naamini muda mzuri utafika suala hili litafikia mwisho''
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger