Kayumba Kuongezwa Kings Music ya Alikiba...


Msanii Kayumba amefunguka kuhusu ukaribu wake na msanii Alikiba pamoja na jina lake kutajwa sana kujiunga na kundi la Kings Music Records ambayo inamilikiwa na msanii huyo.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Kayumba amesema yote kheri  kwa sababu Alikiba ni mtu ambaye anamkubali sana pia anamsapoti hivyo ikitokea nafasi yupo tayari kufanya nae kazi.

"Ukimzungumzia Alikiba ni msanii mkubwa ndani na nje ya Tanzania,  Pia ni mmoja kati ya kaka zangu ambao wananikubali na kunisapoti na ukaribu wetu ulikuja kutokana na muziki, ikifika wakati wa kufanya biashara tutazungumza nitaangalia sehemu ambayo kutakuwa na maslahi kwangu na kutanikuza kama atanipa nafasi nipo tayari na nitaitumia vizuri" amesema Kayumba 
That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments