9/23/2020

Kessy Atumika Kuiua YangaALIYEWAHI kuwa beki wa Yanga, Hassan Kessy anatarajia kutumika kuhakikisha anaimaliza timu yake hiyo ya zamani kutokana na jukumu alilopewa na kocha wake wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila.


 


Mtibwa Sugar inatarajiwa kuikaribisha Yanga Septemba 27, katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro ikiwa ni mchezo wa nne wa Ligi Kuu Bara iliyoanza kutimua vumbi Septemba 6.


 


Akizungumza na Championi Jumatano,Katwila amefunguka kuwa, anatarajia kuuweka muziki kamili katika mechi hiyo akiwemo Kessy kuhakikisha hawatoi nafasi kwa wapinzani wao kupachika mabao licha ya wapinzani wao kuwa na nyota wa kigeni.
“Mechi yetu na Yanga itakuwa ngumu hakuna asiyejua, wana nyota wengi wa kimataifa lakini haitutishi, tunachokiangalia ni kuhakikisha tunafanikiwa kushinda katika mechi hii muhimu kuweza kupata pointi tatu katika ardhi ya nyumbani.


 


“Wachezaji wangu wote wapo vizuri, sina majeruhi hata mmoja, natarajia kuwa na kikosi bora katika mchezo huo, ambapo Kessy atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza katika mchezo huo, naamini uwepo wake utaongeza nguvu kwa kushirikiana na wachezaji wengine ili kuibuka na pointi tatu,” alisema Katwila.


 


Aidha alimalizia kwa kusema kuwa, wanachohitaji ni kuona timu yake inafanikiwa kumaliza ligi katika nafasi tatu za juu kwa kupata matokeo mazuri katika mechi za awali za mzunguko wa ligi.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger