Kigwangalla Aeleza Alivyokuwa Anauza Vitumbua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla, amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliokulia katika mazingira ya kawaida na alikuwa akizunguka mitaa ya Nzega akiuza Vitumbua na jojo.


Dkt Kigwangalla ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 2, 2020, Mjini Nzega Mkoani Tabora, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mji huo, wakati mgombea urais wa chama hicho Dkt Magufuli alipopita hapo kunadi sera na kuomba kura kwa wana Nzega.

"Mimi nimezaliwa na kukulia katika viunga vya Mji huu ni mtoto wa kawaida kabisa kutoka familia ya kawaida kabisa ya kiswahili, nimezunguka katika Mitaa ya Nzega nikiuza vitumbua na Jojo, nikifanya shughuli za kawaida kabisa ambazo kwa kiasi kikubwa zinafanywa na wananchi ambao siku hizi wanaitwa wanyonge", amesema Dkt Kigwangalla.

Awali Dkt Kigwangalla amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake kwa kumpa nafasi mbalimbali za uongozi Serikalini ikiweno nafasi ya Naibu Waziri wa Afya, pamoja na nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad