Kigwangalla Akoleza Bil. 20 za Simba Akimtaja Mo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amesema hana tofauti wala chuki na Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’,  kama ambavyo wengi wanafikiria baada ya kuhoji juu ya uwekezaji wake wa Tsh bilioni 20.

Wikindi iliyopita Kigwangalla alizua mijadala katika mitandao ya kijamii muda mchache baada ya kutangazwa kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez ,ambaye ametwaa nafasi iliyoachwa na Senzo Mazingiza aliyetimkia Klabu ya Yanga.

Akitolea ufafanuzi, Kigwangalla amesema; ”Sina matatizo na Dewji, yule ni rafiki yangu na pia alikuwa mbunge mwenzangu, nilishafanya naye biashara, suala la mkopo wa pikipiki wala siyo tatizo kwa kuwa nilimkopa, lakini alileta uswahili, mwanzo alikubali, baadaye alikataa.

“Lakini baadaye nilinunua kwa kuwa nilikuwa nataka kupeleka jimboni kwangu ili kukimbizana na muda, hivyo kama ningekuwa na chuki naye basi nisingerudi tena kununua bidhaa kwake.

“Suala la kuhoji Tsh bilioni 20 nilishawahi kufanya hivyo tangu mwezi Januari, hivyo baada ya kuona mambo kama hayaendi vile inavyotarajiwa, ilibidi niulize kwa kuwa niliona wanamuajiri Barbara ambaye ni mfanyakazi kutoka Taasisi ya Mohamed Dewji, maana yake hapo kutakuwa na tatizo kwa kuwa mchakato haujakamilika.”

Kigwangalla amesisitiza kwamba baada ya kuona baadhi ya wanachama na mashabiki wa Klabu ya Simba  wamekasirika wakiamini anataka kumfukuza mwekezaji wao, sasa atakaa kimya ila ukweli utakuja kujulikana.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad