Kilichotokea Baada Dkt Magufuli Kucheza SingeliUkipitia kwenye mitandao ya kijamii kuna clip moja ambayo inatrend sana kwa sasa ikimuonyesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kucheza wimbo wa Singeli wa msanii Sholo Mwamba.

Sasa kupitia kipindi cha Planet Bongo msanii huyo wa singeli amenyoosha maelezo kuhusiana na kilichoendelea baada ya Rais Magufuli kucheza muziki wake kwenye kampeni za Urais mkoani Singida.

"Kikubwa ni kumshukru Mungu kwa sababu sijategemea kama ingekuwa vile, kwa uwezo wa Mungu ameamua kunibariki kijana wake, nilishawahi kuota kwenye ndoto zangu kwamba siku moja nitaimba halafu Rais atacheza"
"Baada ya pale nilizungumza na Rais Magufuli kupitia simu ya Ikulu Mawasiliano kwa Gerson Msigwa na amesema amependa nilichofanya na nilivyovaa kitamaduni, pia ametusihi kuongeza ubunifu"
"Tangu nilivyomaliza show pale nimeshindwa kulala mpaka sasa hivi, yaani siamini kama ni mimi kweli ambaye Rais amecheza wimbo wangu, kikubwa zaidi namshukuru Mungu na mashabiki zetu waendelee kusapoti muziki wa singeli"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments