9/09/2020

Kiongozi mwingine maarufu wa upinzani akamatwa BelarusMaafisa nchini Belarus wamemkamata mjumbe wa mwisho wa ngazi za juu wa baraza la upinzani waliokuwa wamebaki huru, ikiwa ni hatua ya kimfumo ya kuyamaliza maandamano yaliyodumu mwezi mmoja dhidi ya Rais Alexander Lukashenko. 

Wakili Maxim Znak, mwanachama wa Baraza la Uratibu lililoundwa na upinzani kusimamia mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo aliyekaa madarakani kwa miaka 26 sasa, alichukuliwa katika ofisi ya baraza hilo na watu wasiojulikana waliokuwa wamefunika nyuso zao. 


Waendesha mashitaka wa Belarus wameanzisha uchunguzi wa jinai dhidi ya wanachama wa Baraza la Uratibu, wakilituhumu kwa kuhujumu usalama wa taifa kwa kudai uhamisho wa madaraka. Wanachama wengine kadhaa walikamatwa na wengine wakafukuzwa nchini.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger