Ticker

6/recent/ticker-posts
.

KMC yataja kilicho nyuma ya ushindi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREUONGOZI wa KMC umesema kuwa kikubwa kinachowabeba ndani ya Ligi Kuu Bara ni wachezaji kujituma na kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

Ushindi wa jana Septemba 21 walioupata KMC mbele ya Mwadui FC kwa kushinda mabao 2-1 kumewafanya wawe nafasi ya kwanza wakiwa na pointi zao 9 kibindoni baada ya kucheza mechi tatu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kila mchezaji anatambua majukumu yake na kutimiza kwa wakati jambo linalowapa matokeo chanya.


"Wachezaji wanatambua kwamba nini kinahitajika ndani ya timu na wao hesabu zao ni kuona wanapata ushindi hiyo ndiyo furaha yao pia.


"Kwa kufanya hivyo kunawafanya wawe na nguvu katika kupambana na kupata matokeo na hicho ndicho ambacho kinatokea, tupo na tunazidi kupambana zaidi na zaidi," amesema.


KMC ilianza kushinda kwa mabao 4-0 mbele ya Mbeya City na ikashinda mabao 2-1 mbele ya Tanzania Prisons na jana ilishinda mabao 2-1 mbele ya Mwadui FC, Uwanja wa Mwadui Complex. 

Post a Comment

0 Comments