Kocha Mserbia Apewa Kibarua Kigumu Yanga SC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KOCHA Mkuu mpya wa Yanga Mserbia, Zlatko Krmpotic amepewa masharti makubwa kwenye mkataba ambayo anatakiwa kuyafanya msimu ujao unaoanza kesho.


 


Kocha huyo alitua Jumamosi iliyopita tayari ameanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho kilichoweka kambi yake kwenye Kijiji cha Avic Town huko Kigamboni na kesho ataanza kukaa benchi kwa mara ya kwanza wakati timu hiyo itakapovaana na Prisons kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.


 


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kocha huyo katika mkataba wake wa miaka miwili aliousaini amewekewa malengo ambayo ili aendelee kubakia, ni lazima achukue mataji yote watakayoshiriki timu hiyo.




Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kati ya mataji hayo, la Ligi Kuu Bara ndiyo limepewa kipaumbele lengo ni kuhakikisha wanawapoka watani wao wa jadi, Simba pamoja na FA.


 


“Kocha mpya Zlatko ana kibarua kigumu katika msimu huu, hiyo ni kutokana na mkataba wake aliousaini ambao unamtaka achukue mataji yote watakayoshiriki Yanga.




“Hivyo, kama anataka kuendelea kubakia Yanga basi aipe mataji timu hiyo na kati ya taji ambalo wanalitaka la ubingwa wa ligi ambalo GSM ndio wanalitaka zaidi,” kilisema chanzo hicho.Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga ambaye pia ni Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said alisema: “GSM tumechukua dhamana yote ya msimu huu ya kuhakikisha tunauchukua ubingwa wa ligi, hiyo ndiyo sababu tumebeba dhamana ya kusimamia usajili wote wa msimu huu kwa kuhakikisha tunasajili wachezaji waliokuwa na bora wataoipa ubingwa Yanga.”


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad