9/01/2020

Kocha wa Zamani Kenya Afunguka Kuhusu Mchezaji wa SIMBA "Onyango Hana Mvuto Kwa Mashabiki"Kocha wa zamani wa Kenya, Harambe Stars, Adel Amrouche raia wa Ubelgiji amesema Onyango ni kati ya mabeki bora aliowahi kuwanoa na wanaombeza wataona tofauti pale atakapoanza kucheza.

Amesema kawaida Onyango hana mvuto kwa mashabiki badala yake ana mvuto mkubwa kwa watu wa ufundi kwa maana ya makocha.

Onyango amejiunga na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya kwa kandarasi ya miaka miwili na mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya Vital’O ya Burundi ambapo Simba ilishinda mabao 6-0 Uwanja wa Mkapa

”Ni miongoni mwa wachezaji wazuri ambao hawavutii nje ya uwanja lakini uwezo wao ni ndani ya uwanja hivyo nina amini atafanya makubwa ambayo wengi hawataamini.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger