9/09/2020

KOCHA YANGA ASEMA, CARLIONHOS HAKUWA FITIKOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga Zlatko Kmpotic ameeleza sababu za kutomtumia kiungo wao nyota kutoka Angola Carlos Carlinhos kwenye mchezo Wa kwanza ligi kuu vodacom Tanzania bara dhidi ya Wajela jela Tanzania Prisons kuwa mchezaji huyo bado hayupo fit.


Katika ukurasa wa kijamii wa Yanga umeleza kuwa kocha huyo mpya amewahakikishia wanayanga kuwa wakati wa mchezaji huyo utafika na tapata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.


Aidha kocha huyo raia wa Serbia ameeleza kuridhishwa na uwezo wa nyota huyo hodari, Muhimu anahitaji afikie fitness inayotakiwa.


"Sina shaka na uwezo wake ni mchezaji mzuri ana kipaji cha hali ya juu, Lakini nadhani anahitajika kuimarika zaidi, Hayuko tayari kucheza dakika 90, Alimalizia kwa kusema sio yeye tu wako wengine pia tunawaangalia baada ya muda nafikiri tutakuwa na kikosi imara."amesema kocha Zlatko Kmpotic."


Katika muendelezo wa Ligi kuu Yanga ina kibarua cha kuwavaa Mbeya City Septemba 13, 2020 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar as Salaam majira ya Saa moja jioni akiwa mwenyeji wa mchezo huo .


Ikumbukwe katika mchezo uliopita Yanga ililazimishwa sare ya kufungana gol i1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na kuvuna alama moja, huku Mbeya city wao wakiambulia kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa vijana Wa Kinondoni KMC FC.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger