9/26/2020

Lamine Moro: Yanga Waongo, Sijasaini Mkataba
LAMINE Moro ni mmoja kati ya mabeki wa kati wenye uwezo mzuri kwenye Ligi Kuu Bara na yeye anakipiga kwenye kikosi cha Yanga.Mei mwaka huu Yanga ilitangaza kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja beki huyo ambao utaisha mwaka 2023.


 


Moro ambaye mara nyingi hapendi kuzungumza sana ni mzaliwa wa Accra, Ghana alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Buildcon FC, Zambia lakini kumbuka aliwahi pia kupita Simba na kufanya majaribio.


 


Msimu huu Yanga ina mabeki wa kati wazuri ambao wanaweza kuleta ushindani mkubwa kwenye kusaka kikosi cha kwanza ambao ni Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Said Juma Makapu na Lamine mwenyewe.
Sasa Championi Jumamosi, limefanya mahojiano na mlinzi huyu mwenye umbo kubwa na mrefu, kuhusiana na ishu mbalimbali ikiwemo maisha yake ndani ya Yanga.


 


Moro amefunguka vitu vingi ikiwemo ishu ya kukana kusaini mkataba ambao Yanga walitangaza kuwa wamemuongeza jambo ambalo limemkera. Kumbuka mlinzi huyu ana bao moja alilofunga dhidi ya Mbeya City ambapo Yanga walishinda 1-0.


 


ULIJISIKIAJE ULIPOTUA YANGA“Nilifurahi. Napenda kuushukuru uongozi wangu kwa kuweza kunisajili ili niweze kuitumikia Yanga.
MSIMU HUU YANGA INA MABEKI WAKALI WA KATI, UMEJIPANGAJE?


“Kila mmoja ana uwezo wake na hata wao walipokuwa wanasajiliwa waliangalia upungufu uliokuwepo na mpaka kusajili mabeki wengine.“Kila mtu ana nafasi yake na uwezo wake na kukiwa na ushindani wa namba, utanifanya hata mimi kuzidisha bidii ili kupata nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza.


UNGEPENDA KUCHEZA NA NANI BEKI YA KATI?


“Kiukweli siwezi kusema nani nafurahi kucheza naye kwani sisi wote ni wachezaji na nina imani mpaka mchezaji awe ndani ya Yanga basi ana vigezo vyote na ubora, mimi nafurahi kucheza na mchezaji yeyote yule ndani ya Yanga.


 


UMEFUNGA BAO MOJA, VIPI MASHABIKI WATEGEMEE ZAIDI?


“Kiukweli nimejipanga vizuri sana msimu huu namuomba sana Mungu niwe na afya njema na mtayaona zaidi ya haya“Sikuwahi kuwa mfungaji katika maisha yangu ya soka ila nimejiona nina uwezo wa kufunga na nitajitahidi kutupia mabao mengi msimu kadiri nitakavyokuwa napata nafasi.


 


UNADHANI YANGA INAWEZA KUBEBA UBINGWA?


“Ubingwa ni malengo ya kila timu hivyo hata sisi tunatamani sana kuwa mabi ngwa pia ukia ngalia timu yetu kwa sasa ina wachezaji wazuri, tuta pam bana kup ata kile tulichopanga.


 


UMEJIP-ANGAJE KUWA-KABILI SIMBA OKTOBA 18?“Kiukweli siwezi kusema kama nitacheza au la ila huo ni uamuzi wa kocha nani aanze na nani aingie kipindi cha pili kwani mabeki wote ni wazuri.


 


UNADHANI YANGA ITAIFUNGA SIMBA?“Kiukweli hakuna anayependa kushindwa hivyo hata na sisi tuna imani tutaibuka washindi dhidi ya watani wetu wa jadi, cha zaidi ni kuombeana heri kila kitu na kitaonekana siku hiyo.


 


BEKI GANI MKALI KWA SASA BONGO?“Mimi sipendi uongo mabeki wote wa timu ya Simba wako vizuri hata kama sio timu yangu ila nasema ukweli kuwa Simba wana mabeki wazuri na wenye viwango vya juu.


 


UPO TAYARI KUBADILISHA URAIA WAKO ILI UCHEZE TAIFA STARS?“Ndio nipo tayari nikipata nafasi ya kuchaguliwa basi nitabadilisha na nina hamu sana ya kucheza Taifa Stars, kwa kuwa sijawahi kuitwa kwenye timu yangu ya taifa ya Ghana ya wakubwa.


 


KITU GANI UNAKICHUKIA SANA YANGA?“Nachukia sana uongo wanaoongea hasa kwa upande wa viongozi


 


WALIKUDANGANYA NINI?


“Wamedanganya kwa wadhamini kuwa eti nimesaini mkataba mpya wakati ni uongo. Mimi sijaingia mkataba mpya na Yanga na wasiponipa ninachostahili kwa kweli nitaondoka.“Juzi kocha aliniita na kuniambia ananihitaji sana ila mimi nataka kuondoka mana timu nyingi zinanihitaji.


 


WAKIKUPA NINI UTABAKI?


“Kusema kipi nataka ni siri yangu na uongozi, ila wasipokitimiza nitaondoka, siwezi kutaja timu ninayotaka kwenda ila nina timu nyingi zinanihitaji ila mimi naona upande wa viongozi


 


WALIKUDANGANYA


“Wamedanganya kwa wadhamini kuwa eti nimesaini mkataba mpya mpya na Yanga ninachostahili kwa kweli “Juzi kocha aliniita mkataba wenye manufaa kwangu ni timu kutoka Afrika ya Kusini na wa Misri hivyo nitachagua wapi ila asilimia za mimi kubaki Yanga ni ndogo sana.


 


IKITOKEA SIMBA WAKIKUTAKA UPO TAYARI KWENDA?


“Walikuwa wananitaka (kwenye usajili wa dirisha kubwa mwaka huu) ila wakinitaka sasa nipo tayari kwenda kuitumikia timu yao. Mimi ni mchezaji na sio shabiki hivyo naenda sehemu yenye manufaa na maisha yangu.


UNAIONAJE SAFU YA USHAMBU-LIAJI YA SIMBA?“Wako vizuri ila hata wa Yanga wako vizuri ni suala la muda tu kwa kuwa kwetu wachezaji hawajakaa pamoja muda mrefu ukilinganisha na wale wa Simba.


 


JE, UNAWAOGOPA?“Hapana siwaogopi.


NIPANGIE KIKOSI CHAKO CHA KWANZA YANGA“Kiukweli siwezi kupanga maana kila mtu yupo kwa ajili ya kucheza.”


 HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger