9/28/2020

Lissu Mwendo Mdundo na Kampeni Adai Hajapokea Malalamiko yoyote Kutoka NEC

 


Mgombea Urais kupitia,Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kuwa hajapokea malalamiko yoyote kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), yanayohusu mwenendo wa ufanyaji wa kampeni zake, huku akidai kuwa hatohudhuria suala lolote linalohusiana na kampeni zake.


Lissu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, yakiwa yamepita masaa kadhaa tu tangu NEC, ilipotoa tamko la kwamba, imemuandikia barua mgombea huyo kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuikashifu NEC kwamba itaiba kura zake, pamoja na madai ya kwamba mgombea urais wa CCM, Dkt. Magufuli atakutana na wakurugenzi wa Halmashauri hivi karibuni.

"Sijapokea malalamiko yoyote juu ya jambo lolote linalohusiana na kampeni za uchaguzi mkuu huu kutoka NEC, sijapokea wito wowote kuhusu jambo lolote linalohusiana na kampeni za uchaguzi mkuu huu kutoka NEC, sitarajii kuacha kampeni ili kuitikia wito wa mitandaoni wa mtu yeyote", ameandika Lissu.

Jana Septemba 27, 2020, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Charles Mahera, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Arusha, alisema kuwa Lissu alitoa tuhuma hizo kwenye mikutano yake ya kampeni mjini Musoma kati ya Septemba 25 na 26 mwaka huu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

2 comments:

 1. Kweli, wewe ni mkosefu wa Adabu na Nidhamu.

  Tundu, usijifaye Hamnazo.
  Tumekuona na kukusikia. katika mwenendo wako wote wa upotohaji/ Uongo uliokithiri/ uchonganishi / Unafikiuliovuka mipaka na Ahadi hewa kwa wana Usalama na sisi Wananchi tunao kujaga kukusikiliza Porojo zako.

  Tafadhali fika Djedengwa haraka iwezekanavyo kujieleza kwa mujibu wa taarifa na wito uliopewa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Swadakta mdau.

   Amani yetu ni jukumu letu Watanzania wote.

   Hatuto mruhusu yeyote wakiwemo
   wanasiasa uchwara kuivuruga au
   kuiteteresha kwa milimita moja kwa Maslahi yao Binafsi dhidi yetu tusiopungua millioni 60.

   TUNDU,CHEZEA PESA KAMA UNAZO (LOFA) NA SIVYO AMANI YETU NA UTULIVU WETU KWA AJILI YA NJAA YAKO NA KULA KWAKO.

   Tanzania ni Salama na Tulivu.
   DUMISHA HILO NA SI VINGINEVYO.

   UHAMASISHAJI WAKO NI POTOSHI.

   Delete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger