Magufuli Alivyokomesha Fukuza Fukuza ya wachimbaji Wadogo Wadogo Wanapogundua Madini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa katika kipindi chake cha uongozi wachimbaji wa wadogo wa madini wamekuwa wakipewa leseni pale wanapogundua maeneo yenye dhahabu badala ya kufukuzwa.



Amesema hayo leo Septemba 9 akiwa anaongea na wananchi wa Geita nakusema kuwa tofauti na siku za nyuma wachimbaji wadogo wanahesabiwa kama wawekezaji nchini.

"Siku za nyuma ilikuwa ukishagundua dhahabu wanafukuzwa wanakuja wakubwa ukipata mahali unafukuzwa wanakuja wengine tukasema hapana! wakigundua wanabaki palepale na wanapewa leseni na wao waweze kutajilika kwasababu tunawahesabu wao kama wawekezaji", alisema Rais Magufuli.

Aliendelea kusema,"Tumejitahidi kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwatengea maeneo, kufuta ama kupunguza viwango vya kodi walivyokuwa wanalipa na kuwapatia mafunzo na mitambo yakuendesha shughuli zao za uchimbaji"

Aidha Rais magufuli amesema kuwa waliweza kuunda sheria zilizoweza kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini na kuanzisha soko kubwa makoani hivyo kupelekea uuzwaji wa madini kwa wachimbaji wadogo kupanda kutoka kilo 337 hadi kilo 4656.29 kwa mwaka 2019.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad