Makamu wa Rais Afghanistan ashambuliwa kwa bomuMakamu wa Rais wa Afghanistan Amrullah Saleh amenusurika kwenye jaribio la mauaji dhidi yake baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bomu, ambalo limewauwa karibu watu 10 na kuwajeruhi wengine kadhaa, karibu na mji mkuu, Kabul.


Afghan VP Amrullah Saleh escapes deadly bomb attack in Kabul | News | Al  Jazeera


Mara tu baada ya mlipuko huo, Saleh, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Taliban, alisema alikuwa njiani kwenda ofisini kwake wakati msafara wake ulishambuliwa.


Kabul Bomb: Deadly Blast Targets Afghan Vice-President Amrullah Saleh


Amesema yupo salama licha ya kupata majehara madogo tu ya kuungua usoni na mikononi. Mwanawe wa kiume ambaye alikuwa naye kwenye gari, pia yuko salama.


Tariq Arian ni msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan. Shambulizi hilo lililaaniwa mara moja kama jaribio la kuuhujumu mchakato wa kutafuta amani nchini Afghanistan, lililofanywa wakati serikali ikijiandaa kuwatuma wajumbe wake nchini Qatar kwa mazungumzo yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu na Taliban

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments