9/29/2020

Mambo sita kuhusu Wema Sepetu kutimiza miaka 30

 


Msanii na nyota wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu siku ya leo Septemba 29 anatimiza miaka 30, ambapo kupitia instagram yake amepost picha mbalimbali zikimuonesha kujipongeza, haya hapa ni mambo sita ya kufahamu kuhusu siku yake hii muhimu ya kuzaliwa.


Msanii wa filamu Wema Sepetu


1. Wafuasi 'followers' wengi instagram


Wema Sepetu ndiye msanii wakike mwenye wafuasi wengi kuzidi wasanii wengi wa kike Bongo ambapo ana followers milioni 7.7 huku akiwa ame-follow watu 515, hii inatokana umaarufu wake na kupendwa na watu wengi.


2 .Miss Tanzania 2006


Wema Sepetu alivishwa taji hilo mwaka 2006 baada ya kuwashinda warembo kama Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, na Lisa Jensen ambao walifika tatu bora katika kumtafuta mrembo bora Tanzania.


3. Tuzo ya msanii bora wa kike 


Wema  amewahi kuchukua tuzo ya sinema zetu April 2018, aliipata tuzo hiyo kupitia kinyanganyiro cha 'Peoples Choice' wakati wa kumchagua muigizaji bora wa kike na kuwashinda waigizaji kama Riyama Ally na Rachel Kayuga.


4.Orodha ya wapenzi aliowahi kutoka nao


Inasemekana kuwa Wema Sepetu ni miongoni mwa msanii wa kike ambaye amewahi kutoka na wasanii maarufu nchini kama vile Marehemu Steven Kanumba, Idris Sultan, Bob Junior, Mr. Blue, TID, Calisah  na wengine wengi na baadae kuachana nao.


5. Kukosa mtoto 


Moja kati ya vitu vinavyomtesa Wema Sepetu ni kukosa mtoto na kwa bahati mbaya sana watu wengi wamekuwa wakitumia udhaifu huo kumshambulia mitandaoni ila binafsi anaamini ipo siku atapata mtoto wake mwenyewe na kumlea.


6. Kupunguza mwili 


Watu wamekuwa wakimuhukumu kuhusu muonekano wake wa sasa ambapo wanasema anachukiza, amepoteza mvuto na kuonekana kama amekonda baada ya kufanya surgery ya kupunguza baadhi ya nyamanyama za mwili wake ambazo zilikuwa zinamfanya aonekane ana mwili mkubwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger