Manara Afunguka Ukweli Chama Kuondoka SimbaMSEMAJI wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kuhusu tetesi za mchezaji wao, raia wa Zambia, Clatous Chama, ambaye anadaiwa kuwa mkataba wake uko karibuni kumalizika hivyo ataondoka klabuni hapo huku akihusishwa kujiunga na mahasimu wao Yanga SC.


 


Manara amesema hayo leo leo Septemba 24, alipotembelea Studio za +255 Global Radio akiambatana na Idara ya Habari ya klabu hiyo na kupiga stori kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na klabu hiyo na mipango yao.


 


“Hii ni mara yangu ya tatu kutembelea media houses Tanzania tangu niingie kwenye kazi hii, tumekuja kuwaeleza mashabiki wetu na Watanzania mambo ambayo Simba SC tumepanga kuyafanya.


 


“Viongozi wa Simba SC wataongea na uongozi wa Clatous Chama kuangalia namna ya kuongeza mkataba wake ambao unaisha Julai 2021, nimesikia Yanga SC wanasema watamchukua, pale atacheza na nani? Pasi za visigino atampa nani?


 
 


“Ili Chama aweze kucheza vizuri anahitaji timu inayomiliki mpira, akienda Yanga SC atachezaje? Kwanza hawana pesa ya kumnunua, mkataba wake ni dola milioni moja, Yanga wana hiyo pesa? Mashabiki wa Simba SC wasibabaishwe na propaganda za mitandaoni, viongozi wana uchungu na timu hawawezi kuruhusu aondoke.


 


“Walichokifanya Yanga SC kuhusu kufungua duka la jezi sisi tulishafanya miaka minne iliyopita, sisi tuna malengo makubwa sasa hivi na tuko mbali sana, duka sio ishu kwetu.


 


“Sisi tunashindana na Al Ahly na Casablanca FC kwenye mitandao ya kijamii, unatulinganishaje na Yanga SC? Chukua akaunti yetu ya Instagram, linganisha na ya kwao, chukua akaunti yao rasmi, viongozi na akaunti za wachezaji wao hawatufikii.


 


“Simba SC ina asilimia 70 ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/2021, Azam FC ina asilimia 25, Yanga SC asilimia 1 na timu nyingine zilizobaki wanapigania asilimia 4 zilizobaki,” amesema Manara.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments