9/02/2020

Marekani kutoshiriki katika Mpango wa Chanjo dhidi ya Covid-19Marekani imetangaza kuwa haitahusika katika mpango wa ulimwengu unaolenga kutengeneza, kutoa na kusambaza chanjo dhidi ya Covid-19

Kulingana na habari katika gazeti la "Washington Post", Msemaji wa White House Judd Deere amesema kuwa Marekani haitashiriki katika Mpango wa Chanjo dhidi ya Covid-19 (Covax), ambao unaratibiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Akisisitiza kuwa Marekani itafanya suala la chanjo peke yake, Deere, amesema

"Marekani itaendelea kushirikiana na washirika wake wa kimataifa kuvishinda virusi, lakini haitajishirikisha na mashirika ya kimataifa chini ya ushawishi wa Shirika la Afya Duniani na Uchina."

Utawala wa Donald Trump umetangaza mnamo Mei 29 kwamba umemaliza uhusiano wake na WHO kwa madai kwamba "shirika hilo lilifanya maamuzi yaliyoathiriwa na China katika kupambana kwake na janga hilo".

Mikutano inafanywa na zaidi ya nchi 170 zilizo chini ya mpango wa Covax, ambao unakusudia kuharakisha juhudi za kutengeneza chanjo ulimwenguni, kuwezesha nchi zote kufaidika na chanjo na kuwafanya watu walio katika hatari kubwa wanufaike na chanjo wakiwa wa kwanza.

Mashirika mengi na nchi nyingi zikiwemo nchi washirika wa Marekani kama Ujerumani na Japan, wameunga mkono mpango huo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger