9/13/2020

Maskini Ommy Dimpoz Asimulia Alivyokata Tamaa Baada ya Kuambiwa Ana Kansa ya Inni

NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIFIKISHA LEO TENA TAREHE 13 MWEZI WA TISA KWANI NI SIKU YANGU YA KUZALIWA LAKINI KUNA KISA KIMOJA KILINITOKEA MWAKA JANA NATAKA NIWAHADITHIE.KILITOKEA KIPINDI NIPO KWENYE SAFARI YANGU YA MATIBABU... BAADA YA KUFANYIWA OPERATION MBILI KUBWA ILE YA KWANZA SOUTH AFRICA NA ILE YA PILI UJERUMANI MUNGU AKAJAALIA NIKAPATA AFYA TENA MPAKA NIKAANZA KURUDI KWENYE SHUGHULI ZANGU ZA KAWAIDA NIKATOA MPAKA NYIMBO YA NI WEWE NA ZINGINE,SASA UKAFIKA MUDA NATAKIWA KURUDI TENA UJERUMANI HOSPITALI KWENDA KUCHEKIWA TENA HALI YANGU INAENDELEAJE...NILIVYOFIKA UJERUMANI NIKAANZA VIPIMO NA MAJIBU YAKAJA MAZURI SO DAKTARI AKANIRUHUSU NIRUDI NYUMBANI TANZANIA JAPO KUNA KIPIMO KIMOJA KILIKUWA BADO MAJIBU HAYAJARUDI ILA DAKTARI WANGU AKANIAMBIA ATANITUMIA MAJIBU KWA EMAIL KWAHIYO HAKUNA HAJA YA KUSUBIRI BASI NIKAFURAHI SANA NIKAJIANDAA NA SAFARI YA KURUDI NYUMBANI KWANI PIA NILIKUWA NARUDI ILI NIJIPANGE NA SAFARI YA KWENDA SAUDIA ARABIA UMRA ( UMRA NI IBADA YA WAISLAM INAFANYIKA MAKKA) SASA WAKATI NIPO AIRPORT LIMEBAKI KAMA LISAA LIMOJA KUPANDA NDEGE GLAFLA NIKAPIGIWA SIMU NA DAKTARI WANGU AKINIOMBA NISIONDOKE KWANI KUNA DHARURA IMETOKEA NIKASHTUKA SANA 😳 IKABIDI NICANCEL TIKETI NIKAPANDA TAX KURUDI HOSPITALI KUFIKA DAKTARI AKANIAMBIA MAJIBU YA KIPIMO YALIYOBAKI YAMEKUJA INAONEKANA KUNA DALILI SIO NZURI KWENYE MAPAFU YAKO SO ITABIDI UBAKI KWA MWEZI MMOJA MAANA ISIJE KUWA NI KANSA JAPO HATUNA UHAKIKA 😢 BASI NIKAISHIWA NGUVU NIKASEMA MUNGU WANGU YANI KUUMWA KOTE HUKU TAKRIBANI MIAKA 2 BADO TENA KUNA MAMBO YA KANSA KIUKWELI NILIKATA TAMAA...SASA NIKAMUULIZA DAKTARI VIPIMO VITAGHARIMU KIASI GANI? AKANIAMBIA LAZIMA NIFANYIWE OPERATION NDOGO ILI WAWEZE KUTOA KINYAMA KWENYE MAPAFU YANGU KWAAJILI YA KUPIMA KUJUA TATIZO KWA KINA (Biopsy) KWAHIYO ITABIDI NILAZWE KAMA KWA WIKI MBILI SO GHARAMA YAKE ITAKUWA EURO ELFU 25 SAWA NA MILIONI 68

NIKASHTUKA SANA KUSIKIA HIZO GHARAMA NIKAMWAMBIA DAKTARI WANGU KIUKWELI HIZO PESA NI NYINGI SANA MAANA NILIENDA KWAAJILI YA CHECK UPS SO SIKUJUA KAMA INGETOKEA SWALA LA KULAZWA TENA JAPO NILITAMANI KUJUA NINA TATIZO GANI? AKANIULIZA SASA TUNAFANYAJE NIKAMWAMBIA ACHA NIRUDI AFRICA NIKAJIPANGE THEN NTARUDI,AKANIAMBIA SIWEZI KUKURUHUSU MAANA LISIJE KUWA NI TATIZO KUBWA INABIDI NIJUE. AKANIAMBIA NIMSUBIRI KWA DAKIKA CHACHE NJE YA OFISI YAKE,BAADA YA MUDA KIDOGO AKANIITA HUKU AKINIANGALIA KWA HURUMA AKASEMA NIMEJADILIANA NA TIMU YANGU TUMEAMUA KUKUFANYIA MATIBABU BURE 😳NIKASHTUKA SANA SIKUAMINI MAANA SIKUWA NA BIMA YA AFYA HALAFU NI NGUMU SANA KUTIBIWA BURE. BASI KESHO YAKE NIKAFANYIWA TENA ILE OPERATION NIKALAZWA KWA ZAIDI YA WIKI NIKISUBIRI MAJIBU KAMA NI KANSA AU LAA!! NIKAWA KILA MUDA NAINGIA GOOGLE KUANGALIA KANSA YA MAPAFU ATHARI ZAKE NIKAZIDI KUKATA TAMAA NIKAJUA SAFARI HII SITOBOI.BASI SIKUMOJA WAKAJA MADAKTARI KAMA 10 WAMENILETEA MAJIBU 😳🙆🏽‍♂️ NIKASHTUKA SANAAA NIKAJUA TAYARI LAKINI KWA BAHATI NZURI WAKANIAMBIA MAJIBU YAMEKUJA SIO KANSA ILA KUNA BACTERIA WAMEONA HIVYO KUNA DAWA WATANIPA NIWE NATUMIA.NIKAPIGA GOTI NA KUMSHURU MUNGU THEN NIKARUHUSIWA SASA KURUDI AFRICA: MARA WAKATI NAJIPANGA NA SAFARI NIKAPATA SIMU KUTOKA KWA @victorwanyama AMBAYE TULIKUWA TUNAWASIANA MARA KWA MARA AKINIJULIA HALI AKANIAMBIA KAMA MAJIBU YAMEKUWA POA BASI NJOO MADRID UJE KUCHEKI MECHI YETU YA FAINALI YA UEFA, WALIKUWA WANACHEZA TOTTENHAM NA LIVERPOOL DAH NIKAFURAHI SANA NIKACHUA NDEGE MPAKA MADRID MAANA ILIKUWA NI LISAA LIMOJA KUTOKEA UJERUMANI NILIVYOFIKA FAMILIA YAKE IKANIPOKEA TUKAJIANDAA KWENDA UWANJANI, TULIVYOFIKA UWANJANI KUNA MASHABIKI WENGI WALIKUWA HAWANA TICKET ZILIKUWA NI HADIMU SANAAAA BASI KUNA MZUNGU MMOJA AKASEMA ANATAKA TICKET NA YUKO TAYARI KUTOA POUND ELFU 10 SAWA NA MIL 30 YA KIBONGO 😳😳 NIKAWAZAAA SANAAAA JE NILAMBE KIBUNDA NIUZE YANGU VICTOR ANIONE MSWAHILI AMA NITIMIZE NDOTO YA KUANGALIA FAINALI KUBWA KAMA UEFA BASI NIKAPIGA MOYO KONDE NIKAENDA KUANGALIA MECHI, KWA BAHATI MBAYA KINA VICTOR WAKAFUNGWA 😢 @victorwanyama ALIVYOJUA KAMA NILIKATAA KUUZA TICKET AKANICHEKA SANA NA KUNIITA FALA 

HAPPY BIRTHDAY TO ME
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger