Max Rioba: Kwa sasa mimi sio meneja wa Hamisa wala Wema, P Square watakuwepo kwenye tamthilia yetu, Batuli kamkosea sana WemaAliyewahi kuwa meneja wa @hamisamobetto @maxrioba ameweka wazi kuwa kwa sasa yeye sio meneja wa @hamisamobetto tena wala sio meneja wa @wemasepetu ila anafanya nao kazi tu.


Max amedokeza kuwa katika Tamthilia yake ya WE MEN wameanza mazungumzo na wasanii wa nje kama P Square kutoka Nigeria Casper Nyovest kutoka Afrika Kusini na Saut Soul kutoka Kenya ili waanza kufanya nao kazi kwenye Tamthilia hiyo.


Lakini pia Max akiwa kama mtu wa karibu wa @wemasepetu ametoa maoni yake kuhusu kinachoendelea kati ya wasanii wa Bongo Movie Wema Sepetu na @officialbatuliactress kujibizana mitandaoni hadi kupeleka Batuli kumpost Wema na kuandika maneno ambayo yalionekana kutomfurahisha Wema, Max ametoa maoni yake na kusema kinachotakiwa ni heshima Batuli hakupaswa kuandika maneno kama yale kwa msanii mwenzake.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments