Mbunge wa Kenya Akamatwa kwa "Kumtukana Rais Uhuru Kenyatta"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mvutano kati ya Rais Kenyatta na naibu wake umesababisha mgawanyiko katika chama tawalaImage caption: Mvutano kati ya Rais Kenyatta na naibu wake umesababisha mgawanyiko katika chama tawala
Mbunge mmoja wa Kenya amekamatwa kufuatia matamshi aliyotoa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wikendi iliyopita, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Johanna Ng’eno anatuhumiwa kwa kutumia maneno ya matusi kumdhalilisha rais, kulingana na taarifa ya gazeti la Daily Nation inayonukuu ripoti ya polisi.

Kanda ya video inayomuonesha mbunge huyo akizungumzia mgogoro kati ya rais Kenyata na naibu wake William Ruto imezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii.

Mbunge huyo anasikika akimwambia rais avunje serikali ikiwa ameshindwa kufanya kazi na bwana Ruto.

Hali ya taharuki ilishuhudiwa wakati wa kukamatwa kwa mbunge huyo wa Emurua Dikirr, katika eneo la bonde la ufa huku tukio hilo likioneshwa moja kwa moja katika ukurasa wake wa Facebook.

Baada ya kukamatwa kwa bwana Ng'eno, naibu wa rais aliandika ujumbe katika Twitter yake akisema "viongozi wanapaswa kujizuia na kuepuka kutumia lugha ya matusi dhidi ya Wakenya wengine".
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad