Mbwana Samatta Aanza Kazi Fenerbahce

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mshambuliaji wa timu ya soka nchini Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkataba wa miaka minne kutoka Aston Villa.

Klabu hiyo imeandika katika mtandao wake kwamba imemuongeza nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania katika kikosi chake kwa mkataba wa miaka minne.



Mchezaji huyo aliyeshinda taji la mfungaji bora mara kadhaa nchini Ubelgiji kabla ya kujiunga na Aston Villa nchini Uingereza atahudumu katika klabu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja kabla ya kuandikisha kandarasi ya kudumu ya miaka minne.

Ripoti kutoka Istanbul zinasema kwamba mshambuiaji huyo atavalia jezi nambari 12 mgongoni katika klabu yake mpya.

Fenerbahce inayoshiriki katika ligi kuu ya Uturuki siku ya Ijumaa ilimzindua Samatta rasmi ikichapisha kanda ya video katika akaunti yake ya Twitter.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad