Mbwana Samatta Aanza Kuisoma Namba Villa....Aliyesajiliwa Juzi Atupia BaoMSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, ameanza kupata changamoto ya kuwania namba katika kikosi cha kwanza cha Aston Villa huku usajili mpya katika nafasi hiyo, Ollie Watkins akianza kumkimbiza kwa kufunga bao katika mechi yake ya kwanza kuichezea timu hiyo.


Samatta aliingia akitokea benchi dakika ya 66, kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao pekee, Watkins, wakati wakishinda 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Villa Park juzi.


Watkins aliyesajiliwa majira haya ya joto akitokea Brentford kwa ada iliyoweka rekodi Aston Villa, kiasi cha pauni milioni 28 ambazo zinaweza kuongezeka na kufikia pauni milioni 33, alifunga bao hilo pekee katika dakika ya 16. 

Kiungo Mmisri Mahmoud Ahmed Ibrahim maarufu Trezeguet, ndiye aliyemtengenezea bao hilo Watkins, ambaye kwa kiwango alichoonyesha kinaonyesha anakwenda kuwa tishio kwa Samatta katika kuwania namba kikosini hapo.Wakati Ligi Kuu England ilianza rasmi juzi, Jumamosi, timu hizo zilikubaliana kucheza mechi ya kirafiki kutokana na mechi zao za ufunguzi za ligi hiyo kuahirishwa.


Manchester United ilikuwa ianze na Burnley kwenye Uwanja wa Turf Moor na Aston Villa walitakiwa kuwafuata Manchester City kwenye dimba la Etihad, lakini mechi hizo ziliahirishwa ili kuzipa nafasi zaidi timu hizo za Jiji la Manchester kujiandaa kutokana na kushiriki michuano ya klabu barani Ulaya hadi hatua za mwishoni.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments