9/21/2020

Mbwana Samatta Akubali Yaishe Aston Villa, Atimukia Timu HiiBaada ya Mzee Ally Pazi kutoa baraka zote kwa mwanaye, Mbwana Samatta kufanya maamuzi kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari nchini Uturuki, imeripotiwa nahodha huyo wa Taifa Stars amekubali kujiunga kwa mkopo waMbwana Samatta akubali muda mrefu na Fenerbahce

Kwa mujibu wa gazeti la Takvim huko nchini Uturuki, imeripotiwa Aston Villa klabu ambayo anaichezea Samatta na Fenerbahce wamefikiana makubaliano ambayo yatamfanya mshambuliaji huyo kuitumikia miamba hiyo ya Uturuki kwa mkopo wa msimu mzima

Imeelezwa mkopo huo utakuwa na kipengele cha kununuliwa moja kwa moja mara baada ya kumalizika mwakani. Mkataba wa Samatta na Aston Villa ambayo alijiunga nayo kwa Pauni 8.5 millioni mwanzoni mwaka huu (Januari), unatarajiwa kumalizika mwaka 2024.

Ripoti hiyo, ilieleza Samatta anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Fenerbahce ambacho wikiendi ijayo kitacheza dhidi ya Galatasaray ambayo aliwahi kuichezea Muafrika mwenzake, Didier Drogba.

Awali Besiktas ambayo na yenyewe ni klabu kutoka Uturuki iliripotiwa kuongoza mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Tanzania ambaye ameripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamewekwa sokoni na klabu yake.

Aliyekuwa akiongoza Oparesheni ya kumng’oa Samatta huko Villa Park ambako ni wazi inaonekana nafasi yake ya kucheza msimu ujao ni finyu alitajwa kuwa ni Emre Kocadag ambaye ni miongoni mwa watu ambao wapo kwenye bodi ya Besiktas

Licha ya kuwa Fenerbahce wameonekana kuipiga bao Besiktas, Alhamisi ya wiki iliyopita ziliibuka pia tetesi nyingine ambazo ziliihusisha Bromwich Albion F.C.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Sun, iliripotiwa kwamba West Bromwich Albion F.C. wapo kwenye mchakato wa kuipiga bao Fenerbahce kwenye kinyang’anyiro cha kuinasa saini ya mshambuliaji huyo wa Aston Villa

Ilielezwa Kocha wa West Brom, Slaven Bilic ana mpango wa kukiimarisha kikosi chake ikiwemo katika idara ya ushambuliaji kutokana na kuanza kwao vibaya mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England dhidi ya Leicester City, walipoteza kwa mabao 3-0

VILLA YAPIGILIA MSUMARI

Baada ya kupata saini ya mchezaji bora wa Ligi daraja la Kwanza ‘Championship’, Ollie Watkins ambaye alikuwa akiichezea Brentford, Aston Villa imeendelea kuimarisha kikosi chake kwenye idara yao ya ushambuliaji kwa kunasa kifaa kingine.

Safari hii, wameenda Ufaransa ambako wamemnasa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Bertrand Traoré ambaye ni raia wa Burkinafo aliyekuwa akiichezea Olympique Lyonnais.

Aston Villa wanatarajiwa kucheza leo, Jumatatu mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu England wakiwa nyumbani kwenye uwanja wao wa Villa Park kucheza dhidi ya Sheffield United katika mchezo uliopita ambao ulikuwa wa Carabao dhidi ya Burton , Samatta aliishia kukaa benchi.

BONGO ZOZO AIBUKA

Mzee wa kupiga fujo zisizoumiza, Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo amemwomba Samatta kama anaondoka Aston Villa basi aichague Bromwich Albion badala ya Fenerbahce.

“Napenda kuendelea kumuona akicheza England, haitakuwa mbaya kama atajiunga na West Brom, bado ninaimani na uwezo wa Samatta anaweza kuwafunga wazungu hawa hadi akili iwakae sawa,” alisema.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger