9/21/2020

Mchungaji Amuua Mkewe Kwa Kumtandika Risasi Saba...CCTV Zarekodi Tukio Zima


Pichani mchungaji huyo wa nchini Ghana kwa jina la Sylvester Ofori(35) ametiwa mbaroni nchini Marekani anakoishi baada ya kumuua mkewe huyo kwa jina la Barbara Tommey(27). Amemuua kwa kumfyatulia risasi saba nje mbele ya ofisi anazofanyia kazi mkewe huyo

Camera za cctv ndio zimenasa tukio hilo ingawa sababu za kumuua mkewe hazijajulikana mara moja. Lakini kwa mujibu wa taarifa baadhi ya ndugu wa mke huyo walishamshawishi ndugu yao huyo aachane na mwanaume huyo baada ya kugundua mke alikuwa ananyanyaswa muda mrefu na mume(domestic violence) lakini mwanadada huyo akawa anavumilia kuona pengine mume angebadilika

Ukiacha cemera za Cctv zilizonasa tukio, mwanamke mmoja kwa jina la Lisa aliyeshuhudia tukio la mauaji hayo amesema lilikuwa tukio la kinyama sana kwake kushuhudia kwani mwili ulimtetemeka sana. Amesema amesikitika Barbara kuuliwa kwani alipokuwa akienda kwenye ofisi yao alikuwa mtu mkarimu sana na kumhudumia vizuri

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger