9/15/2020

Membe: Afya Yangu imeimarika, Sasa nipo Tayari kwa Kampeni za Urais Naanzia TaboraMgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Bernard Membe amesema afya yake imeimarika na yupo tayari kwa ajili ya kuanza tena kampeni za Urais.
Membe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amewaatarifu wanachama na Watanzania wote kuwa anatarajia kuwasili leo Septemba 15 nchini Tanzania kutokea Dubai.

“Afya yangu imeimarika na sasa nipo tayari kwa kampeni za Urais,  inayoanzia Tabora wiki hii hadi Oktoba 26”, amesema Bernard Membe.
“Wana ACT-Wazalendo na Watanzania wenzangu wote, Kesho Jumanne ya tarehe 15 Sept saa 8.40 mchana, nitatua Dar es salaam nikitokea Dubai”, ameongeza.

Awali Membe alizinfua kampeni zake katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

1 comment:

 1. Membe huyu. MEMBE.
  Membe kapitwa na Mengi kwa siku mbili alizotoroka.

  Sasa kwa taarifa yako Membe. Kuna maazimio ambayo huyajui NI kwamba Chama kitashirikiana na Chama kingine kuunga mkono wagombea panapo kubalika na WAO kukubalika.

  Ushauri wangu NI bora ukuta e na viongozi wako WA Juu wanaotaka kuwaunga mkono we zako WA Ubwabwa na Uhulu.

  CMM kiboko Yao...!!! Piga KELELE kwa MCC yakeeee.

  MBEMBE HIYO MBEMBE... Shush a Tanga uende Muheza.

  Pole Sana na Ugonjwa.. Pumzika na Fata Ushauri WA Daki Tari wakati wote. Nyie wote wagonjwa na Hali zenu Za kiafya na Dozi mnazo tumia haziwaruhusu kwani Afya zenu NI bora kuliko ikulu.

  IKULU SIO HURUMA KWA WAGONJWA. NI BORA KWENDA MIREMBE KUENDELEA NA MATIBABU NA MOI MIFUPA.

  ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger