Meneja Amlaumu Mondi ‘Kumhujumu’ Tanasha Dona Kisa Wimbo Mpya wa Zuchu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MENEJA wa msanii na mtangazaji Tanasha Donna, Jamal Gadaffi,  akiwa kwenye mahojiano alidai kuwa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, anatumia nguvu nyingi kwa msanii Zuchu ili kumhujumu Tanasha ambaye ni mama wa mtoto wake huku akidai kuwa jambo hilo si jema kulifanya.

“Mondi anatumia nguvu nyingi sana kwa Zuchu, ili amfunike mzazi mwenziwe… unaona live tu Diamond anavyomsukuma Zuchu si kawaida tu ni sababu tu ya Tanasha, kutaka kuwalinganisha hao wawili. Lakini mimi naona kibiashara ni sawa, lakini mwisho wa siku ni mzazi mwenzake, asingempa wakati mgumu,” alisema Jamal.


Alisema kuwa anapenda kazi ya msanii Zuchu lakini mtindo wake wa muziki ameutoa na kuiga kwa Tanasha

“Kwanza mimi Zuchu namkubali sana, yuko vizuri Zuchu, napenda kazi yake, ila kitu ambacho nilipost ni kwamba, kuna wimbo wa Tanasha ambao ulivuja, unaitwa Ride, amemshirikisha Khaligraph Jones. So kuna miondoko flani hivi kaitumia Zuchu mimi nikahisi mbona kamuiga mwenzake.

“Watu ambao niko karibu nao WCB ni kama Romy Jones, Richardo Momo. Na hata kumcheki mtu kama Richardo Momo si hoja, lakini mimi nimeacha tu ipotelee kwenye mitandao, because it’s not that big. Mimi ni style tu mimi nilikuwa naongelea. Style flani hivi Tee anatumianga. So hiyo ati ni kitu kikubwa ati tutapigia hadi management,” Jamal alisema.

Pia alidai kuwa Tanasha hajawahi kulalamika kwa jambo lolote kuhusu Diamond, “Hajawahi kulalamika hata siku moja, lakini ni vitu mimi naona sio lazima hata kuambiwa, jinsi kunavyokwenda, sio lazima eti yeye aniambie kuko hivi.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad