Mke Wa Carlinhos Adatishwa Na Mashabiki Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MREMBO  Vanessa ambaye ni mke wa kiungo mpya wa Yanga, Carlinhos, raia wa Angola, amekuwa akionyesha mahaba yake waziwazi kwa staa huyo kwenye mitandao ya kijamii.


Lakini juzi alionekana kukunwa na mashabiki wa Yanga kwa jinsi walivyompokea mumewe wakati akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea kwao Angola.

Vanessa alitupia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikionyesha jinsi Carlinhos alivyopokewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga, kisha akaandika maneno haya:“Mpenzi wangu…tumshukuru Mungu kwa namna gani? Kwa baraka hiyo, nina furaha hukuacha kujiamini hata kila mmoja alipokoma kukuamini.

Ni Mungu pekee ndiye anayejua nyakati za usiku tulizotumia kwenye maombi.

“Siku zote nilikuambia wakati wako utafika, kipaji, unyenyekevu siku zote zinaendelea kuwa nawe. Ni Baba tu wa mbinguni anayeweza kufanya hayo.

Tunafurahi kujua kwamba umepokewa vizuri katika namna hii kwenye nchi ambayo haijulikani kabisa kwetu.“Mungu aendelee kuwa pamoja nawe, atembee nawe, usimsahau Mungu mpenzi…nakutakia mafanikio endelevu katika hatua hiyo mpya. Fanya kile unachojua kukifanya kwa ubora; KUCHEZA MPIRA.” Wapendanao hao wawili wana watoto watatu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad