9/01/2020

Mo Dewji Amsaka Shabiki Aliyechaniwa Jezi UwanjaniMWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji,  anamsaka shabiki wa Simba aliyechaniwa jezi yake na watu wanaoaminiwa kuwa wapnzi wa Yanga kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi na video ya tukio hilo kusambaa mitandaoni.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter,  Mo Dewji ameweka leo Septemba 1, 2020, video ya shabiki huyo na kuandika ujumbe kwamba mpira ni ushindani, utani na si uadui.

“Namtafuta shabiki huyu wa Simba aliyechaniwa jezi, nataka kukutana nae. Mpira ni Ushindani, Mpira ni Utani, Mpira sio Uadui!” umesema ujumbe huo.

Tukio la kuchaniwa jezi na kuzongwa na mashabiki hao limezua mijadala mitandaoni na watu wakilaani kitendo hicho ambacho si cha kiungwana michezoni.

Uongozi wa Yanga tayari umetoa taarifa ya kulaani jambo hilo na kusema kitendo hicho si cha kiungwana na hawakiungi mkono.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger