9/22/2020

Morrison Ageuka Kinara Wa Nidhamu Simba SCMENEJA Mkuu wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hapati usumbufu wowote kutoka kwa kiungo mshambuliaji wake mpya Mghana, Bernard Morrison.


Mghana huyo akiwa anaichezea Yanga inasemekana alikuwa akiwafanyia vioja na usumbufu uongozi wa timu hiyo kabla ya kujiunga na Simba kwenye msimu huu.

Kati ya vioja na usumbufu ambao aliwahi kufanya akiwa na Yanga ni kuondoka kambini bila ya ruhusa kutoka kwa uongozi wakati timu hiyo ikiwa kwenye hoteli moja Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Rweyemamu alisema kuwa amefurahishwa na nidhamu kubwa anayoendelea nayo Morrison tangu ajiunge na timu hiyo kwenye msimu huu.Rweyemamu alisema kiungo wake huyo anaishi vizuri na ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake, benchi la ufundi na viongozi wakati wakiwa kambini.

“Morrison mbona yupo freshi hana tatizo na mtu, anaishi vizuri na wachezaji katika maisha ya tofauti nje na ndani ya uwanja, hivyo kwangu najisikia furaha.

“Tangu Morrison alipojiunga na Simba hakuwahi kuleta usumbufu wowote zaidi ya kutoa ushirikiano kwa wachezaji wenzake kwa kila jambo linalotokea ndani na nje ya kambi.

“Morrison ni mcheshi anayependa kujichanganya na wachezaji wenzake zaidi hajawahi kuleta usumbufu wowote ndani wala nje ya kambi na kwangu ana nidhamu ya hali ya juu,” alisema Rweyemamu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger