Mpinzani Aliyenyweshwa Sumu Atoka Hospitali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KIONGOZI wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny, ameonekana kwa mara ya kwanza hadharani baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya mjini Berlin ambako alikuwa anatibiwa kutokana na sumu inayoua mishipa ya fahamu.


 


Mwanasiasa huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 44 amekaa hospitalini mjini Berlin kwa siku 32, 24 kati yake akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, kabla ya madaktari kujiridhisha kuwa hali yake imeimarika vya kutosha kuweza kumruhusu. Timu yake imesema hata hivyo, kwamba atasalia nchini Ujerumani kwa muda kuendelea na matibabu ya uangalizi.


 


Katika ujumbe wa mtandao wa Instagram ulioambatanishwa na picha yake, Navalny amesema alikuwa anajifunza kurejesha urari wake kwa kusimama juu ya mguu mmoja, na amewashukuru madaktari wa hospitali ya Charite ya mjini Berlin kwa matibabu waliyompatia.


 




Ujerumani Yashusha Pumzi


Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert, amesema serikali imepata ahueni kutokana na kuruhusiwa kwa Navalny, lakini amekataa kutoa taarifa juu ya wapi alipo na kwa muda gani ataendelea kuwepo Ujerumani kabla ya kuomba hifadhi, akisema hilo litategemea mamlaka za uhamiaji.


 


Serikali ya Ujerumani inasema vipimo vilivyofanywa nchini Ujerumani, Ufaransa na Sweden vimeonyesha kuwa alipewa sumu ya kemikali aina ya Novichok, ambayo inaua mishipa ya fahamu. Mataifa ya Magharibi yametaka maelezo kutoka Urusi. Seibert amesema Ujerumani na washirika wake wa Umoja wa Ulaya wataendelea kuishinikiza Urusi kutoa maelezo.


 


”Bado tunaendelea na mawasiliano na majadiliano na washirika wetu wa Ulaya, na tutazidi kufanya hivyo, ili kuweza kufikia hitimisho juu ya namna ya kutathmini taarifa za Urusi kuhusu kesi hii na namna tunavyopaswa kujibu,” amesema Seibert.




Kremlin Yashikilia Msimamo Wake


Serikali mjini Moscow imesema bado haijaona ushahidi ya uhalifu na imekataa kuanzisha uchunguzi kamili mpaka sasa, badala yake imeanzisha uchunguzi wa awali, huku ikulu ya Kremlin ikikanusha kuhusika kabisa na kadhia hiyo. Hata hivyo, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Navalny yuko huru kurejea Moscow.


 


”Ni habari njema ikiwa kweli mgonjwa anaendelea vyema. Tunamtakia uponaji wa haraka. Kuhusu kurejea kwake Moscow – kama ilivyo kwa kila raia wa Urusi, ana haki ya kufanya hivyo wakati wowote,” alisemaPeskov.


 


Siku ya Jumanne, gazeti la Ufaransa la Le Monde liripoti kwa kunukuu vyanzo, kwamba Rais wa Urusi, Vladmir Putin alisema Navalny huenda alikunywa sumu mwenyewe kwa sababu isiyojulikana.


 


Lakini Peskov amesema gazeti hilo lilipotosha mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Putin na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na kwamba ripoti hiyo haikuwa sahihi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad